Breaking News

BAADA YA KUTISHA KWENYE UZINDUZI SASA FILAMU YA BAHASHA KUANZA KUONEKANA SINEMA LEO




BAADA YA KUTISHA KWENYE UZINDUZI SASA FILAMU YA BAHASHA KUANZA KUONEKANA SINEMA LEO

Ukisikia neno Rushwa unapata picha gani kwenye fikra zako? Unadhani Rushwa inahusisha pesa kubwa kubwa tu!! Leo hii katika Kumbi za Sinema za Mlimani City unaletea Filamu ya “Bahasha”iliyozinduliwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Sinema wa Mlimani City.

Filamu hii ya BAHASHA imeandaliwa na Ubalozi wa Uswisi na Uholanzi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) inayozungumzia madhara yanayojitokeza katika sehemu mbalimbali inayosababishwa na rushwa. Kupitia filamu hii tunamuona mwenyekiti wa mtaa wa Mtakuja, Kitasa akichukua fedha kwa ajili ya kuwashawishi kamati yake watie saini na kuuza eneo la wazi kujengwa eneo ambalo watoto wamekuwa wanalitumia kwa ajili ya michezo, likiwa karibu na shule ambapo katika jengo hilo walilojenga liliweza kuleta madhara ya uharibufu ya miundo mbinu ya maji, kubakwa kwa mtoto wake wa kike Hidaya na changamoto zingine. Tizama kipande kuifupi hapa chini na usikose kuifuatilia filamu hii.



Ratiba ya filamu hii kuonesha ni kama inavyoonekana kuanzia leo Septemba 7 kuanzia saa 6 mchana, saa 10 jioni na saa 2 usiku katika Kumbi za Century Cinemax Mlimani City.

No comments